Date: 
13-02-2026
Reading: 
Mathayo 11:25-30

Ijumaa asubuhi tarehe 12.02.2026

Mathayo 11:25-30

25 Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.

26 Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

27 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Neno la Mungu li hai;

Yesu alikuwa amehubiri na kufundisha kwenye miji na vijiji, lakini wapo ambao hawakuamini. Ukisoma kuanzia mstari wa 20 hadi 24 Yesu anatoa "ole" kwa miji ambayo haikuanini. Anatabiri hukumu kwa kutokuamini kwao. Lakini Yesu anaendelea kumshukuru Baba yake kwa neema ya Injili ambayo wapo walioiamini.

Somo linaendelea kumuonesha Yesu akiendelea kuhubiri na kuita watu kumfuata, akiwataka wote wenye kulemewa na mizigo kumfuata. Yaani hapa anawaita watu kumwamini kwa njia ya neno lake. Tutaipata raha anayoiahidi Yesu (29) tukikaa kwa Yesu na kulitii neno lake daima. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa