Date: 
14-02-2026
Reading: 
Amosi 8:11-12

Jumamosi asubuhi tarehe 14.02.2026

Amosi 8:11-12

11 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana.

12 Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione.

Neno la Mungu li hai;

Ujumbe huu wa Amosi ulikuja wakati kulikuwa na hali mbaya katika nchi. Njaa ilishamiri, wenye mamlaka na uwezo wakatumia fursa hiyo kuwanyonya wengine. Haki ikakosa, watu wakaishi bila matumaini. Ujumbe wa Amosi ulilenga kuwaonya watu kuacha mara moja vitendo viovu, maana vilimchukiza Mungu. Aliwataka watu kutumia nafasi zao kwa mapenzi ya Mungu kwa kutenda haki.

Nabii Amosi anasema Bwana ataleta njaa katika nchi, njaa ya kulikosa neno la Mungu. Hapa Amosi alikuwa anaonesha kwamba neno la Mungu ni zaidi ya chakula cha mwili. Kwa hiyo ujumbe huu uliwataka watu kuzingatia neno la Bwana ili haki itawale, lakini pia walishike neno kabla siku za kulikosa hazijaja. Nasi tulishike kabla ya mwisho wetu, ili neno hilo lituongoze kuuelekea huo mwisho ulio mzuri. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

 

0784 968650