Date:
18-02-2026
Reading:
Luka 18:31-38
Jumanne jioni tarehe 17.02.2026
Luka 18:31-34
31 Akawachukua wale Thenashara, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii.
32 Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate;
33 nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka.
34 Walakini hawakuelewa maneno hayo hata kidogo, na jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao, wala hawakufahamu yaliyonenwa.
Yesu aiendea njia ya mateso Yerusalemu;
Somo la usiku huu ni taarifa ya Yesu juu ya kufa kwake. Jumapili ya juzi tuliona kwamba Yesu alitoa taarifa hii mara tatu katika Injili zote zinazofanana, yaani Mathayo, Marko na Luka. Yaani katika kila Injili, Yesu alitoa taarifa hii mara tatu. Tuliangalia taarifa zote tatu katika Injili ya Mathayo, maana ndilo lilikuwa somo la mahubiri (Mt 17:22-23). Sasa usiku huu kwa kuwa tunaelekezwa kutafakari Injili ya Luka, tuangalie Yesu alivyotoa taarifa ya kufa kwake mara 3 katika Injili hii;
Taarifa ya kwanza aliitoa hapa;
Luka 9:21-22
21 Akawaonya, akawakataza wasimwambie mtu neno hilo; 22 akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka.Taarifa ya pili;
Luka 9:43-45
43 Wote wakashangaa, wakiuona ukuu wa Mungu. Nao walipokuwa wakiyastaajabia mambo yote aliyoyafanya, aliwaambia wanafunzi wake, 44 Yashikeni maneno haya masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu.45 Lakini hawakulifahamu neno lile, likafichwa kwao wasilitambue; wakaogopa kumwuliza maana yake neno lile.
Taarifa ya tatu ndilo somo la usiku huu (soma tena hapo juu)
Ujumbe;
Yalikuwa ni maandalizi ya Yesu kwa wanafunzi wake, kuwaweka tayari kwa mambo yaliyokuwa yanakuja. Alitaka wajue kuwa atateswa, atakufa na kufufuka. Ni njia ya mateso aliyoiendea kwa ajili wa kuukomboa ulimwengu. Tunakumbushwa kwamba Yesu aliteswa na kufa kwa ajili yetu, basi tutubu na kurejea kwake ili tuwe na mwisho mwema. Amina
Tunakutakia maandalizi mema ya Kwaresma.
Heri Buberwa Nteboya
