Date: 
26-02-2026
Reading: 
Yeremia 3:21-25

Hii Kwaresma 

Alhamisi asubuhi tarehe 26.02.2026

Yeremia 3:21-25

21 Sauti inasikiwa juu ya vilele vya milima, ni kulia kwao na maombi yao wana wa Israeli; kwa kuwa wameipotosha njia yao, wamemsahau Bwana, Mungu wao.

22 Rudini, enyi watoto waasi, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; maana wewe u Bwana, Mungu wetu.

23 Ni kweli, msaada haufai unaotazamiwa kutoka milimani, makutano yenye mshindo juu ya milima; ni kweli, wokovu wa Israeli ni katika Bwana, Mungu wetu.

24 Lakini kitu cha aibu kimeila kazi ya baba zetu tokea ujana wetu; makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao.

25 Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi Bwana, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu ujana wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu.

Katika Yesu kila jaribu lina mlango wa kutoka;

Alhamisi ya leo tunamsoma Yeremia akitoa wito wa kutubu kwa Israeli. Kupitia kwa Nabii Yeremia, Bwana anawaita Israeli kama watoto waasi, akiahidi kuwaponya maasi yao (22). Israeli wanaambiwa kwamba wokovu ni katika Bwana Mungu wao. 

Wito wa kutubu ndiyo tunaokumbushwa katika majira haya. Tufanye yote katika Kristo katika utume wetu, tukizingatia imani ya kweli, toba na msamaha. Tunapotubu Mungu hutusamehe, hivyo ni wajibu wetu kubadilika. Hakikisha kabla hujalala (hujafa) umesamehewa dhambi zako. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa