Date:
04-04-2026
Reading:
2 Wakorintho 5:14-15
Jumamosi asubuhi04.04.2026
2 Wakorintho 5:14-15
14 Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote;
15 tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.
Kwa kupigwa kwake sisi tumepona;
Mtume Paulo anawaandikia watu wa Kanisa la Korintho juu ya kuishi kwa imani katika Kristo Yesu aliyekufa na kufufuka. Paulo anasema upendo wa Yesu unatubidisha kuishi kama yeye. Paulo anakazia kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya wote, ili wote wawe hai katika yeye aliyewaokoa.
Jana tulikumbuka kufa kwa Yesu msalabani. Tuliangalia njia ya mateso aliyoipitia, lakini pia tukaona kwamba ilikuwa ni kwa ajili yetu. Kwa hiyo kama somo la asubuhi hii linavyosema kwamba Kristo alikufa kwa ajili yetu, sote basi tuwe hai katika yeye tukimwamini na kumtumikia daima. Amina
Tunakutakia Jumamosi tulivu
Heri Buberwa
