Date:
22-04-2026
Reading:
Waebrania 13:20-21
Hii ni Pasaka;
Jumatano asubuhi tarehe 22.04.2026;
Waebrania 13:20-21
20 Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,
21 awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.
Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo;
Mwandishi wa waraka kwa Waebrania anamuita Yesu "Mchungaji Mkuu wa kondoo". Anawaombea baraka wasomaji wake, kwamba Mungu aliyemleta Mchungaji Mkuu wa kondoo awafanye kuwa wakamilifu ili wakayatende yaliyo mapenzi yake Kristo.
Mwandishi wa waraka kwa Waebrania anatukumbusha sisi tuliompokea Yesu Kristo kuyatenda yaliyo mema kwa msaada wa Mungu aliyemleta Mchungaji Mkuu wa kondoo. Ni wito wa imani kwetu, na kutenda yatupasayo katika yeye aliyetuita. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa
