Hii ni Pasaka;
Jumanne asubuhi tarehe 12.05.2026;
Warumi 1:8-13
8 Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inahubiriwa katika dunia nzima.
9 Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake, ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma,
10 siku zote katika sala zangu, nikiomba nije kwenu hivi karibu, Mungu akipenda kuifanikisha safari yangu.
11 Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara;
12 yaani, tufarijiane mimi na ninyi, kila mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.
13 Lakini, ndugu zangu, sipendi msiwe na habari, ya kuwa mara nyingi nalikusudia kuja kwenu, nikazuiliwa hata sasa, ili nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine.
Imetupasa kumwomba Mungu siku zote;
Mtume Paulo baada ya salamu, anaanza waraka wake kwa watu wa Kanisa la Korintho akimshukuru Mungu kwa sababu ya Injili kuhubiriwa dunia nzima. Paulo anaomba ikiwezekana asafiri kuelekea Korintho ili akawaone waamini wa huko. Hamu yake ya kuelekea Korintho anaionesha kwa sala akiomba Mungu amuwezeshe.
Tunachoona kwenye somo la asubuhi hii ni Paulo kuhubiri Injili akimtanguliza Mungu kwa kuomba. Anaamini bila msaada wa Bwana hawezi, ndiyo maana anaomba Mungu amuwezeshe kusafiri ili akahubiri. Tabia ya Paulo ya kuomba ni wito kwetu sisi, kwamba tukumbuke kuomba wakati wote maana bila msaada wa Mungu hatuwezi. Tuombe kwa imani, katika jina la Yesu. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
