Date: 
20-05-2026
Reading: 
Warumi 8:26-30

Jumatano asubuhi tarehe 20.05.2026

Warumi 8:26-30

26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.

Mungu utusikie katika kuomba kwetu;

Mtume Paulo anawaandikia watu wa Kanisa la Korintho kwamba Roho Mtakatifu hutusaidia kuomba ipasavyo, maana sisi wenyewe hatuwezi. Paulo anaeleza kwamba Mungu hufanya kazi na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani walioitwa kwa kusudi lake. Paulo anaendelea kukiri kwamba Kristo ndiye mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

Ujumbe wa Paulo ni kwamba siku zote Mungu yuko na watu wake. Roho Mtakatifu ni Mungu, ndiye huwasaidia waaminio kuomba ipasavyo. Yaani huwaongoza watu wake kuomba kwa imani. Anaposema Mungu hufanya kazi na wampendao, maana yake hujibu sala zao wao wamuombao. Tuendelee kumuomba Mungu pekee, tukiwa na hakika kwamba yeye hujibu maombi yetu. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa