Hii ni Pentekoste;
Jumanne asubuhi tarehe 26.05.2026;
Zekaria 12:10-14
10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.
12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.
14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao.
Roho Mtakatifu ni nguvu yetu;
Neno tulilolisoma ni ahadi ya Mungu kumwaga roho ya neema na kuomba kwa wenyeji wa Yerusalemu. Roho hii ya neema ingewaongoza kuelekea ukombozi, yaani kumtazama Bwana ambaye walijitenga naye. Yaani wangeomboleza kwa uchungu kumrudia Bwana, kwa kilio kikubwa mithili ya kufiwa na mzaliwa wa kwanza.
Katika Agano jipya, sehemu hii huangaliwa moja kwa moja kama unabii wa kusulibishwa kwa Yesu Kristo. Injili ya Yohana hunukuu Zakaria 12:10 kupigwa mkuki kwa Yesu;
Yohana 19:37
Na tena andiko lingine lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma.Imani ya Kikristo hutafsiri unabii huu kama kuangalia mbele, yaani mwisho wa historia ambapo taifa la Israeli litamtambua Yesu Kristo kama Mesiya na kutubu dhambi yao ya kumkataa. Ujumbe huu unatujia asubuhi ya leo kutukumbusha kumtazama Kristo kwa imani, ambaye ni Mwokozi wa Ulimwengu. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
