Date: 
04-02-2026
Reading: 
Warumi 7:12-29

Jumatano asubuhi tarehe 04.02.2026

Warumi 2:17-29

[17]Lakini wewe, ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati, na kujisifu katika Mungu,

[18]na kuyajua mapenzi yake, na kuyakubali mambo yaliyo bora, nawe umeelimishwa katika torati,

[19]na kujua hakika ya kuwa wewe mwenyewe u kiongozi wa vipofu, mwanga wao walio gizani,

[20]mkufunzi wa wajinga, mwalimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati;

[21]basi wewe umfundishaye mwingine, je! Hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe?

[22]Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu?

[23]Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati?

[24]Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa.

[25]Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.

[26]Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! Kutokutahiriwa kwake hakutahesabiwa kuwa kutahiriwa?

[27]Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati?

[28]Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;

[29]bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.

Neema ya Mungu yatuokoa;

Bwana Yesu anawapa angalizo Wayahudi kuhusu sheria. Waliifuata sheria kuliko neno la Mungu, hivyo kuwa watu wa maswali kila wakati kuliko tafakari ya neno la Mungu kuhusu sheria husika. Ndio maana anawapa mfano wa tohara, kuwa asiyetahiriwa lakini akaishika torati, anayo nafasi mbele ya Mungu kuliko asiyeshika torati.

Tunapoendelea kuutafakari upendo wa Kristo, tusiwe watu wa kushika sheria na taratibu kuliko neno la Mungu. Haimaanishi tusifuate taratibu, lakini taratibu zituongoze kulishika neno la Mungu. Neno la Mungu liwe ngao yetu, na liwe juu ya kila kitu. Hakuna sheria iliyo juu ya neno la Bwana. Msaada wetu ni katika jina la Bwana 

Aliyeziumba mbingu na nchi

Siku njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

 

0784 968650