Date: 
06-02-2026
Reading: 
Isaya 44:21-22

Ijumaa asubuhi tarehe 06.02.2026

Isaya 44:21-22

21 Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi.

22 Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa.

Neema ya Mungu yatuokoa;

Ujumbe tuliousoma ulikuwa ni ujumbe kwa wana wa Israeli wakiwa uhamishoni kwamba Mungu hakuwa amewasahau. Mungu anaendelea kuwaambia kuwa ameyafuta makosa yao kama wingu zito, na dhambi zao kama wingu, akiwaita kumrudia. Yaani Mungu alikuwa anawapa hakikisho Israeli kwamba alikwisha kuwasamehe dhambi na kuwakomboa. 

Israeli baadaye walitoka uhamishoni na kurudi kwenye nchi yao. Neema ya Mungu ilikuwa juu yao, wakatolewa uhamishoni. Neema hii ipo kwetu hata sasa, kwamba tumeokolewa bure kwa neema ya Mungu. Wajibu wetu ni kumwamini Yesu aliyetuokoa kwa neema, ili atupe mwisho mwema. Amina

Siku njema

Heri Buberwa