Date:
07-02-2026
Reading:
Luka 8:22-25
Jumamosi asubuhi tarehe 07.02.2026
Luka 8:22-25
22 Ikawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga.
23 Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.
24 Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari.
25 Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?
Neema ya Mungu yatuokoa;
Yesu aliwaambia wanafunzi wake wavuke mpaka ng'ambo ya ziwa, wakaondoka kuelekea huko. Sasa wakiwa kwenye maji, Yesu akalala usingizi, ikashuka tufani na chombo kikaanza kujaa maji, wakawa hatarini. Wanafunzi wakamwendea Yesu na kumwamsha wakisema tunaangamia. Yesu akaamka na kuukemea upepo, kukawa shwari. Wanafunzi walibaki kushangaa kwa jinsi upepo na maji vilivyomtii!
Hii ilikuwa inadhihirisha ukuu wa Yesu, kama Mungu mwenye mamlaka. Ndiyo, Yesu alikuwa mwenye mamlaka, ndiyo maana upepo na maji vilimtii! Yesu alikuwa anawaonesha wanafunzi wake kwamba yeye ndiye mwenye mamlaka yote, mbinguni na duniani. Swali alilowauliza Yesu; "Imani yenu iko wapi?". Inatukumbusha kuwa na imani katika Yesu Kristo aliyetuokoa kwa neema. Amina
Jumamosi njema.
Heri Buberwa Nteboya
