Date: 
11-02-2026
Reading: 
Marko 1:29-31

Jumatano asubuhi tarehe 11.02.2026

Marko 1:29-31

29 Na mara walipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana.

30 Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia habari zake.

31 Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawatumikia.

Neno la Mungu li hai;

Asubuhi ya leo tunaona Yesu akiingia kwa Simoni, na kumponya homa mkwe wa huyo Simoni (mama wa mkewe) aliyekuwa hawezi. Homa ilimwacha mama huyu baada ya kuinuliwa na kushikwa mkono na Yesu.

Baraka ya uponyaji ilipatikana baada ya Yesu kuingia nyumbani mwa Simoni. Kumbe tunawajibika kumkaribisha Yesu nyumbani mwetu, mioyonimwetu, kazini kwetu, n.k maana kwa njia ya neno lake tunayaweza mambo yote. Amina

Jumatano njema

 

Heri Buberwa