Date:
20-02-2026
Reading:
2 Wakorintho 7:9-10
Ijumaa asubuhi tarehe 20.02.2026
2 Wakorintho 7:9-10
9 Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote.
10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
Rarueni mioyo yenu;
Mtume Paulo anaonesha furaha yake kwa waamini waliotubu huko Korintho. Anawapongeza watu wa Korintho kwa kuhuzunishwa na dhambi wakaamua kutubu. Paulo anasema walikuwa na huzuni kwa jinsi ya Mungu wakafanya toba na kuupata wokovu.
Ni wito kwetu asubuhi ya Ijumaa ya leo kutafakari njia zetu, na kutubu tukirejea kwa Bwana. Dhambi inatutenga na Mungu, ndiyo maana katika majira haya tunakumbushwa kutubu na kurejea kwa Bwana. Toba hutuondolea huzuni ya dhambi. Tubu sasa urejee kwa Bwana. Amina
Siku njema
Heri Buberwa Nteboya
