Date: 
24-02-2026
Reading: 
Mwanzo 22:15-19

Hii ni Kwaresma 

Jumanne asubuhi tarehe 24.01.2026

Mwanzo 22:15-19

15 Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni

16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,

17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

19 Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba.

Katika Yesu kila jaribu lina mlango wa kutoka;

Jana asubuhi tuliona Mungu akimpa jaribio Ibrahimu la kumtoa Isaka sadaka ya kuteketezwa. Ibrahimu hakuhoji, alifanya kutekeleza mara moja. Yaani aliandaa kuni, akasafiri na Isaka tayari kumtoa sadaka. Alipofika eneo la kutolea sadaka, alimuweka tayari Isaka kumchinja, Mungu akaiona imani yake na kumpa mwana-kondoo kwa sadaka.

Somo la asubuhi hii linaanzia hapo, malaika wa Bwana anamwambia Ibrahimu kwamba kwa sababu hakumzuilia Mungu Isaka, atambariki. Ibrahimu anaahidiwa uzao wake kuwa kama nyota za mbinguni. Kwa kifupi anaahidiwa kuwa Taifa kubwa. Tukiamini na kutenda yatupasayo, baraka za Mungu zinakuwa upande wetu. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa