Date:
27-02-2026
Reading:
Ayubu 2:6-10
Hii ni Kwaresma
Ijumaa asubuhi tarehe 27.02.2026
Ayubu 2:6-10
6 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake.
7 Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.
8 Naye akashika kigae cha kujikunia; akaketi majivuni.
9 Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe.
10 Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Katika Yesu kila jaribu lina mlango wa kutoka;
Ayubu alijaribiwa na shetani akapoteza mali, watoto, mifugo na kila kitu alichokuwa nacho. Somo la asubuhi hii linaonesha mateso zaidi kwa Ayubu, anapigwa majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata kichwani. Akawa anajikuna kwa kigae. Mke wake alimwambia amkufuru Mungu akafe, Ayubu akamwambia kuwa ananena kama wanawake wapumbavu wanenavyo!
Alichokipitia Ayubu ni rahisi kukisoma, lakini katika uhalisia ni hali ngumu sana. Ayubu alishinda majaribu yote yale kwa kumtegemea Bwana. Ujumbe ulioko hapa ni kuwa tutashinda majaribu tukimtegemea Bwana. Amina
Ijumaa njema
Heri Buberwa
