Date: 
04-03-2026
Reading: 
Kutoka 2:11-15

Hii ni Kwaresma 

Jumatano asubuhi tarehe 04.03.2026

Kutoka 2:11-15

11 Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake, akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake.

12 Basi akatazama huko na huko, na alipoona ya kuwa hapana mtu, akampiga Mmisri yule, akamficha ndani ya mchanga.

13 Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana. Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake, Mbona unampiga mwenzako?

14 Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana.

15 Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.

Ukatili upo, tuupinge

Tunaendelea na juma la kupinga ukatili, Musa baada ya kuwa ameokolewa asife wakati wa kuzaliwa anampiga na kumuua Mmisri aliyekuwa anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake. Siku nyingine anataka kuamua ugomvi wa Waebrania wawili, mmoja anamwambia Musa unataka kuniua kama ulivyomuua Mmisri? Musa anajua siyo siri tena, anakimbilia Midiani. 

Tunamuona Musa akileta suluhu kwa kupiga na kuua! Wengi hutumia maandiko ya Agano la kale kama hili la Musa kuua kuhalalisha mauaji na kisasi. Hiyo ilikuwa kwa wakati wake, kwa mazingira yake. Lakini ujio wa Kristo ulileta wokovu kwa njia ya neema ya Mungu. Hivyo kwa neema hiyo yafaa tujiepushe na matendo maovu kama kuua, wizi, dhuluma, utapeli, ubabe na mengi kama hayo. Acha ukatili, maana huo ni uovu. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa