Date:
10-03-2026
Reading:
Isaya 64:8-12
Hii ni Kwaresma
Jumanne asubuhi tarehe 10.03.2026
Isaya 64:8-12
8 Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.
9 Ee Bwana, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
10 Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa, Sayuni umekuwa jangwa, Yerusalemu umekuwa ukiwa.
11 Nyumba yetu takatifu, nzuri, walimokusifu baba zetu, imeteketea moto; vitu vyetu vyote vyenye kupendeza vimeharibika.
12 Utajizuia usiyaangalie mambo haya, Ee Bwana? Utanyamaza, na kututesa sana?
Mazingira ni uhai tuyatunze;
Ni sala ya wana wa Israeli baada ya kuwa wametoka uhamishoni, wanasali wakikiri kwamba wao ni kazi ya mikono ya Mungu. Wanamuomba Bwana asione hasira wala kukumbuka uovu wao. Wanaonba Bwana kuwarejeshea miji ambayo iligeuka jangwa, na Yerusalemu iliyokuwa ukiwa. Wanaendelea kuomba juu ya nyumba ya ibada iliyokuwa imeharibika. Wanamuomba Bwana asinyamaze, asikie na kuwajibu sala yao.
Israeli walitambua ukuu wa Mungu, wakaona njia pekee ya kurejea katika nchi yao na kuanza upya ni kwa kumuomba Bwana tu. Walitambua kuwa nchi yao walipewa na Bwana, ndiyo maana waliomba kwake. Hata sisi, dunia tuliyomo tumepewa na Bwana, hivyo tuitunze ili iwe mahali salama pa kuishi. Amina
Siku njema
Heri Buberwa Nteboya
