Date: 
12-03-2026
Reading: 
Warumi 11: 33-36

Hii ni Kwaresma; 

Alhamisi asubuhi tarehe 12.03.2024

Warumi 11:33-36

33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!

34 Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?

35 Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena?

36 Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

Mazingira ni Uhai tuyatunze;

Mtume Paulo alikuwa anawaambia Warumi kwamba pamoja na dhambi zao wangesamehewa na kuokolewa, yaani walikuwa wanapewa hakikisho la wokovu. Somo linaonesha hekima ya Mungu na maarifa yake, ya kwamba hukumu zake hazichunguziki na hazitafutikani. Paulo anasisitiza kwamba hakuna aijuaye nia ya Bwana, na hana mshauri kama walivyo watu wa duniani. Hivyo ahadi ya Mungu kuhusu wokovu ni timilifu.

Mungu hawezi kulipwa! (35) Mstari wa 36 unamalizia kuonesha kuwa vitu vyote vyatoka kwake na vinarejea kwake. Inatupa ujumbe wa moja kwa moja kuwa sisi sote na dunia tuliyomo ni mali ya Mungu. Yaani tumetoka kwake, na tutarudi kwake. Imani katika yeye ni muhimu ili tuwe na mwisho mwema. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa