Date: 
08-04-2026
Reading: 
1 Wakorintho 15:1-11

Hii ni Pasaka;

Jumatano asubuhi tarehe 08.04.2026

1 Wakorintho 15:1-11

1 Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama,

2 na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure.

3 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;

4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;

5 na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara;

6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;

7 baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote;

8 na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.

9 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.

10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.

11 Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini.

Yesu mfufuka kaa pamoja nasi;

Mtume Paulo anawaandikia watu wa Kanisa la Korintho kwamba Injili aliyowahubiria ni ile ya Yesu Kristo ambaye alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu, akafa, akazikwa na kufufuka siku ya tatu. Paulo anatoa uthibitisho wa Yesu kufufuka akiandika jinsi alivyowatokea watu mbalimbali baada ya kufufuka. Paulo anajenga hoja ya ufufuko wa Kristo kama msingi wa Injili, maana pasipo Yesu kufufuka imani yetu ni bure kama anavyoandika mbele kidogo;

1 Wakorintho 15:14-17

14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.
15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.
17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.

Paulo anawaandikia Wakorintho kuamini katika Yesu aliyefufuka. Paulo hana shaka na Yesu mfufuka, msisitizo wake ukiwa kila aaminiye kuwa na huyu Yesu mfufuka. Tukumbushane kwamba kufufuka kwa Yesu ni hakika, alishinda dhambi na kifo. Yesu mfufuka anatuita daima kuja kwake, kama tunavyokumbushana asubuhi ya leo. Basi tukae kwake daima, leo na siku zote. Amina

Jumatano njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com