Date: 
15-04-2026
Reading: 
Matendo 22: 6-16

Hii ni Pasaka;

Jumatano asubuhi tarehe 15.04.2026;

Matendo ya Mitume 22:6-16

6 Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.

7 Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi?

8 Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi.

9 Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami.

10 Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye.

11 Na nilipokuwa sioni kwa sababu ya fahari ya nuru ile, nikaongozwa na mikono yao waliokuwa pamoja nami, nikaingia Dameski.

12 Basi mtu mmoja, Anania, mtauwa kwa kuifuata sheria, aliyeshuhudiwa wema na Wayahudi wote waliokaa huko,

13 Akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu yangu Sauli, uone. Nikamwinulia macho yangu saa ile ile.

14 Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, na kumwona yule Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake.

15 Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia.

16 Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake.

Yesu Kristo ajidhihirisha kwa wanafunzi wake;

Paulo anasimulia alivyokutana na Yesu akiwa njiani kuelekea Dameski. Alikutana na Yesu, akaambiwa anavyomuudhi Yesu kwa kulitesa Kanisa. Paulo akaongozwa kuingia Dameski, tayari kwa utume. Anaelekezwa kutubu, kubatizwa na kuliita jina la Bwana.

Yesu alijidhihirisha kwa Paulo akamtuma kuhubiri Injili. Paulo huyu leo ndiye tunasoma nyaraka zake. Alifanya kazi iliyotukuka. Yesu anajidhihirisha kwetu leo akituita kumuamini, kumfuata na kumtumikia. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa