Date: 
01-06-2026
Reading: 
Isaya 6:1-7

Jumatatu asubuhi 01.06.2026

Isaya 6:1-7

[1]Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.

[2]Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.

[3]Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

[4]Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi.

[5]Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.

[6]Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu;

[7]akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa.

Mungu mmoja; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Isaya anapata maono, anawaona Maserafi wakimsifu Mungu. Wanaimba Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi. Dunia yote imejaa Utukufu wake. Wanamsifu Mungu na kumpa Utukufu.

Anayesifiwa ni Mungu mmoja, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Huyu ndiye mbingu na nchi zimejaa Utukufu wake. Tunakumbushwa kumwamini na kumsifu yeye aliye juu ya vitu vyote. Tumpe Utukufu tukimshuhudia kwa mawazo, maneno na matendo yetu, tukiwa na toba ya kweli. Amina

Uwe na wiki njema 

 

Heri Buberwa