Date: 
02-06-2026
Reading: 
Nehemia4:1-6

Jumanne asubuhi tarehe 02.06.2026

Nehemia 4:1-6

1 Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi.

2 Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto?

3 Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.

4 Sikia, Ee Mungu wetu; maana tunadharauliwa; ukawarudishie mashutumu yao juu ya vichwa vyao, ukawatoe watekwe katika nchi ya uhamisho;

5 wala usiusitiri uovu wao, wala isifutwe dhambi yao, mbele zako; kwa maana wamekukasirisha mbele ya hao wanaojenga.

6 Basi tukaujenga ukuta; nao ukuta wote ukaungamanishwa kiasi cha nusu ya kimo chake; maana watu walikuwa na moyo wa kufanya kazi.

Mungu mmoja; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Sura ya nne ya kitabu cha Nehemia inahusu kukabiliana na upinzani uliokuwepo katika kutimiza kazi ya Mungu, Nehemia na Wayahudi walipokuwa wakijenga upya ukuta wa Yerusalemu. Walikumbana na dharau, vitisho na fujo za kila aina kutoka kwa adui zao walioongozwa na Sanbalati na Tobia.

Nehemia alipambana na maadui waliotaka ukuta wa Yerusalemu usijengwe kwa sala. Alimuomba Mungu kuwatunza, kuwapa nguvu kuendelea kuujenga ukuta ule. Adui walipofanya shambulio, Nehemia alitumia imani na matendo, akaweka ulinzi kuzunguka eneo la ukuta (mst 9). Asubuhi ya leo Nehemia anatukumbusha kufanya maamuzi sahihi, na kuyasimamia kwa neno la Bwana. Amina

Siku njema

Heri Buberwa 

Mlutheri