Date:
04-06-2026
Reading:
2 Wakorintho 13:11-13
Alhamisi asubuhi 04.06.2026
2 Wakorintho 13:11-13
11 Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
12 Salimianeni kwa busu takatifu.
13 Watakatifu wote wawasalimu.
Ndugu wakae pamoja kwa umoja;
Ni mwisho wa waraka wa pili wa Mtume Paulo kwa watu wa Kanisa la Korintho. Yaani Paulo anamalizia nyaraka zake zote hapa, akiwasihi watu wa Korintho kutimilika, kufarijiana, kunia mamoja, na kukaa na amani. Paulo anaendelea kuwatakia Mungu kukaa ndani yao.
Paulo anawatakia watu wa Korintho neema ya Kristo, upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu katika kukaa kwao pamoja. Korintho wanapewa ujumbe wa kukaa pamoja katika Bwana. Nasi tukae pamoja katika Bwana. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
