Date: 
06-06-2026
Reading: 
Yohana 17:24-26

Jumamosi asubuhi tarehe 06.06.2026

Yohana 17:24-26

24 Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.

25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.

26 Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

Ndugu wakae pamoja kwa umoja;

Inaaminika kwamba Injili ya Yohana sura ya 17 ndiyo sala ndefu ya Yesu aliyosali, iliyoandikwa. Katika sala hii Yesu alikuwa anawaombea wanafunzi wake. Somo tulilosoma ni mwisho wa sala hiyo ambapo Yesu anawaombea wanafunzi wake wawe naye (Yesu) popote alipo na kuutazama utukufu wake. Mstari wa 26 anawaombea wanafunzi wake pendo la Mungu kukaa ndani yao.

Wanafunzi wa Yesu leo ni mimi na wewe. Yesu alipowaombea wanafunzi wake wawe naye, ilikuwa hitaji lake wamwamini, wamfuate na kukaa naye daima. Huu ndiyo ujumbe wangu kwako Jumamosi hii, kwamba tukae na Kristo, pendo la Mungu likiwa ndani yetu, na Yesu akiwa ndani yetu ndipo tutaweza kukaa pamoja kwa umoja. Amina

Jumamosi njema 

 

Heri Buberwa