Azania Front Yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani 2026
Siku ya Jumapili, Machi 8, 2026 ilifanyika ibada ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front. Ibada za aina hii hufanyika kila Jumapili ya kwanza ya mwezi Machi kila mwaka ili kutoa fursa kwa wanawake kuongoza matukio na huduma zote za ibada.
Ibada zote tatu za siku hiyo ziliongozwa na wanawake ambapo neno kuu la siku hiyo lilikuwa ni kuwakumbusha wanawake na washarika wote Kutunza Mazingira.
